Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Ndg. Yanga Makaga amewataka viongozi wote wanaosimamia ujenzi wa vyumba vya Madarasa kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO 19 kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi ili madarasa hayo yaweze kukamilika ndani ya wakati kama maelekezo ya Serikali yalivyotolewa.
Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku mbili yenye lengo la kuhakikisha anajionea uhalisia wa maendeleo ya ujenzi huo.
"Nasisitiza viongozi wote mnaosimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia fedha zilizotolewa dhidi ya mapambano ya UVIKO 19 kuhakikusha mnafanya kazi kwa kasi lakini kwa kuzingatia ubora na viwango vilivyokusudiwa"
Kaimu Mhandisi wa Halmashauri Ndg. Rahim amewataka mafundi wote waliopata kazi za ujenzi wa madarasa hayo kuhakikisha wanafata BOQ pamoja na michoro ya ramani tofauti watajikuta wamejiingiza kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima, kwani kwenda kinyume na mkataba ni kosa kisheria.
Nae Afisa Mipango wa wilaya Ndg. Ndaro Samson amewashukuru wajumbe wa kamati za ujenzi kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati, japo ametoa angalizo la kamati hizo kuwa tayari kupokea mabadiriko katika kutekeleza baadhi ya maelekezo mfano baadhi ya watoa huduma kukosa viambata sahihi kama EFD bali kupitia kamati hizo utararibu mzuri uwekwe ikiwa ni pamoja na mihustasari ili kazi zifanyike kwa wakati na watu wapewe malipo yao kwa wakati kuondoa malalamiko yasiyo yalazima.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.