Wanawake wilayani Sengerema mkoani mwanza wameadhimisha siku ya wanawake duniani ,na kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili pindi wanapoamua kujikwamua kimaisha.
Imeelezwa kuwa zaidi ya kesi 59 za ukatili wa kijinsia hususani wanawake zimeripotiwa katika Dawati la kijinsia wilaya ya Sengerema ndani ya mwezi januari hadi march mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Bi,Chresencia Joseph aliyekuwa mwakilishi wa jeshi la polisi wilayani Sengerema kitengo cha Dawati la kijinsia ambapo amesema matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yameendelea kutokea kutokana na baadhi ya wanaume kutotambua haki ya mwanamke katika jamii na kuwataka watambue kwani mwanamke ni nguzo ya Taifa.
Hata hivyo wanawake hao wameiomba halimashauri ya wilaya ya Sengerema iendelee kufanya Makongamano ya wanawake kila baada ya miezi 6 ili wajifunze mambo mbalimbali muhimu yanayowalenga lengo ikiwa ni kuendana na kauli mbiu ya maadhimisho ya wanawake ya mwaka huu isemayo Tanzania ya viwanda wanawake msingi wa mabadiliko kiuchumi.
Aidha maadhimisho haya yameanza tangu march 1 mwaka huu wilayani hapa ambapo march 6 waliwatembelea wagonjwa katika Hospital teule ya wilaya ya Sengerema na kuwakabidhi mahitaji mbalimbali.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.