Maafisa waandikishaji wa wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema leo Oktoba 8, 2024 wamepewa mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo kuelekea zoezi la uandikishaji wapiga kura litakaloanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.
Msimamizi msaidi wa uchaguzi ndugu Ally Salim kwa niaba ya Msimamizi wa uchaguzi amewataka waandikishaji hao kwenda kufanya kazi ya uandikishaji wapiga kura kwa makini na weledi ili zoezi hilo likamilike kwa mafanikio.
Mapema maafisa waandikishaji hao wamekula kiapo cha utii na utunzaji wa siri mbele ya Kamishna wa Viapo mhe. Christopher Mbuba ambaye pia amewataka maafisa waandikishaji hao kuheshimu viapo hivyo.
Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema yenye vijiji 71 na vitongoji 421 inatarajiwa kuandikisha wapiga kura 209,635.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.