Jumla ya wahudumu wa Afya 184 kutoka vijiji vyote na mitaa ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Maafisa afya wa kata 7 na Maafisa Maendeleo ya Jamii wawili wamekabidhiwa Pikipiki siku ya Jumatatu tarehe 21 Agosti, 2023.
Baiskeli zilizokabidhiwa zina thamani ya Shilingi 46,000,000, na Pikipiki 7za Maafisa afya zina thamani ya shilingi 27,650,000 zikiwa ni fedha za mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSSP) na Maafisa Maendeleo ya jamii wa kata za Busisi na Ibondo wamekabidhiwa Pikipiki 2 kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ili kurahisisha utendaji wa kazi za kila siku.
Akikabidhi pikipiki hizo kwa watoa huduma hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Yusta Mwambembe amewataka watoa huduma hao walionufaika na vyombo hivyo vya usafiri kuhakikisha wanatumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kuleta matokeo chanya katika shughuli za usafi wa mazingira pamoja shughuli za Maendeleo ya Jamii.
Mratibu wa mradi wa Usafi wa Mazingira vijijini Ndugu Abdulahman Mgonja amesema Pikipiki hizo na Baiskeli zilizokabidhiwa kwa maafisa afya na wahudumu wa afya zitaleta matokeo makubwa kutokana na watoa huduma hao kukabiliwa na changamoto za usafiri mara kwa mara wanapohitaji kufanya shughuli za usimamizi wa usafi na mazingira, hivyo amewaomba watumishi hao pamoja na wahudumu kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo wa usafi na mazingira vijijini.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.