Katika kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani Machi 8 mwaka huu imeelezwa kuwa Matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike na wanawake yamepungua kwa kiasi kikubwa Wilayani Sengerema .
Hayo yamebainishwa na Afisa Maendeleo ya jamii ambaye pia ni Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya wanawake katika Halmashauri ya Wilayani Sengerema Bi.Noela Yamo ambapo amesema kuwa ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na wanawake umepungua kutokana na wanawake kuamka na kutambua haki zao za msingi.
Katika suala la usawa wa kijinsia Bi,Noela amesema kuwa wanawake wamejikomboa kwa hatua kubwa kwani kwa sasa hakuna ubaguzi wa masuala ya kijinsia katika jamii.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yanafanyika kila Machi 8 mwaka huu Duniani kote ambapo Kimkoa yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.
Sherehe hizo zimepambwa na kauli mbiu isemayo
“Kuelekea uchumi wa viwanda, Tuimalishe usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa wanawake Vijijini”
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.