Mpango wa kunusuru kaya masikini Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza umezinufaisha Kaya 14476 ambapo walengwa wote wamepata fedha za kuendesha maisha yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole wakati akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema wakati mpango huo wa kunusuru kaya masikini wilayani sengerema ulipoanza ulikuwa unahudumia kaya 17062 na baada ya kufanya uhakiki Kaya zipatazo 2586 ziliondolewa kwenye mpango kwa kuwa ziliingizwa kimakosa na kubakiwa na kaya 14476 zenye sifa.
Mpango huo umekuwa ni mkombozi kwa wananchi wilayani Sengerema ambapo wanufaika wa mpango huo wamepata nufaa mbalimbali ikiwemo kuanzisha swala ufugaji ,wa kuku,mbuzi ,na wengine kujenga nyumba na baadhi yao kusomesha watoto.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Nyampande Justina Alphonce amesema mpango huu umemsaidia kusomesha watoto wake wapata saba alioachiwa na mume wake baada ya kufariki dunia.
Amesema mbali na kusomesha watoto ameanzisha mradi wa ufugaji wa kuku ambao unamsaidia katika mahitaji mbalimbali ya kuendeshea familia na kuimwagia sifa lukuki serikali kwa kuanzisha mpango huo wa kusaidia kaya ambazo watu wake ni masikini.
Justina amezitaka kaya zinazonufaika na mpango huo kujikita katika swala zima la kujipatia maendeleo kwa kuanzisha ufugaji kwa kuwampango huu utamaliza muda wake na watu wasijikita katika swala ufugaji mradi huo utawaacha wakiwa watupu.
Mratibu wa TASAF Wilaya ya Sengerema Malisa Nduga amesema wananchi wamenufaika na mpango huo ambapo walengwa hao wametumia fedha hizo kwa manufaa yao na kujipatia maendeleo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Magesa mafuru amesema mshikamano na usimamizi mzuri wa mradi huo umewasaidia wananchi kujipatia maendeleo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.