Akitoa taarifa hiyo Mratibu wa TASAF wilaya Ndg. Malisa Ndugha, amesema kuwa idadi hiyo imejumlisha idadi ya kaya za zamani pamoja na kaya mpya zilizoingizwa kupitia mpango wa kuingiza vijiji vipya katika mpango ambapo vijiji vipya 36 vimeongezwa na kufanya kuwa na idadi ya jumla ya vijiji 96 ya kuwa sehemu ya eneo la utekelezaji wa mradi ili kuongeza idadi ya wanufaika jambo ambalo wananchi wamelipokea kwa furaha kwani kilikuwa ni kilio cha mda mrefu hasa kwa vijiji ambavyo vilikuwa havimo katika mpango wa malipo.
Katika malipo haya ya kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba kiasi cha shilingi 467,051,761 sawa ongezeko la zaidi za asilimia 50 zimetumika kuwalipa walengwa wa TASAF
Nao wanufaika wa Mpango wa kunusuru Kaya Masikini wameipongeza Serikali hasa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suruhu Hassan kwa namna ambavyo ameonyesha kujali wananchi wa kipato cha chini na kuruhusu kuongezwa kwa vijiji vipya utekelezaji wa mradi kwani idadi kubwa ya wananchi sasa inanufaika na fedha hizo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.