Kampuni ya “Orecop” inayojishughulisha na uchimbaji wa madini katika Halmashauri ya Sengerema imekabidhi mashine ya kufulia nguo aina ya “West Point” yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni moja ikiwa ni moja ya jitihada za kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Afisa Uhusiano, Mbwana akikabidhi msaada huo kwa niaba ya kampuni hiyo ameuomba uongozi wa Halmashauri kuhakikisha msaada huo unakwenda kutumika kama ulivyokusudiwa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema Magesa Mafuru Boniphace akipokea msaada huo ameishukuru kampuni hiyo na kusema, “mashine hii sasa itakwenda itakwenda katika eneo tulilokuwa tumelitenga kwa ajili ya kuwapatia huduma wagonjwa watakaokutwa na maambukizi ya ugonjwa wa Corona katika eneo la Mwabaluhi.
Hata hivyo amewatoa hofu wananchi wa Sengerema kwa kusema mpaka sasa mji wa Sengerema ni shwari na salama na mpaka sasa ninavyoongea hatuna mgonjwa wa corona, hivyo ndugu zangu wananchi tuendelee kupiga kazi kama ambavyo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuri amekuwa akitutaka watanzania kupiga kazi na kuachana kuwa na hofu juu ya Corona.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.