Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza imeridhishwa na ubora wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambapo pia wameitaka Halmashauri ya Sengerema kuongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Utawala ili lianze kutumika.
Akiongea wakati wa ziara hiyo leo (22.05.2022), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Lushinge (smart) amesema ubora wa miradi hiyo unatokana na usimamizi mzuri chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya, Halmashauri na CCM Wilaya ya Sengerema ambapo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema hivyo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
"Miradi hii tuliyoitembelea leo ina thamani kubwa ikikamilika italeta manufaa makubwa kwa wananchi wetu, hivyo tunampongeza sana Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua fedha hizi zije zitekeleze miradi hii Sengerema" amesema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amepongeza jitihada za Wilaya za kuwaletea wananchi maendeleo ambapo pia amesema kukamilika kwa ujenzi uwanja wa mpira wa Miguu utakuwa ni wa manufaa kwa wananchi na ujenzi wa uwanja huo ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya awamu ya sita hivyo ameahidi kuleta timu ya Pamba jiji na timu zingine za ligi kuu ili uwanja huo utumike kama chachu kwa vijana wa Sengerema.
Mkuu wa Mkoa amepongeza usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ambapo amesema kwa sasa miradi ya Sengerema inakamilika kwa ubora na kwa wakati.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema, Mark Agustine Makoye amesema kujengwa kwa uwanja wa mpira wa miguu wa Mnadani ni ishara ya uwepo wa viongozi wazuri katika Wilaya, hivyo amempongeza Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mbunge wa jimbo la Sengerema kwa kuja na wazo la ujenzi wa uwanja huo ambao pia ni chanzo cha mapato ya Halmashauri.
Miradi iliyokaguliwa na Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza ni pamoja na mradi wa Maji Nyasigu- Lubungo - Ngoma kata ya Igalula, Ujenzi wa daraja la Bugakara, Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Ujenzi wa jengo la Mamlaka ya Mapato Wilaya ya Sengerema na Ujenzi wa uwanja wa Michezo Mnadani yote ikiwa na jumla ya bilioni 20.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.