Kamati ya Siasa mkoa wa Mwanza imetembelea miradi mbalimbali ya maendele katika Halmashauri ya wilaya ya Sengerema na kujione jinsi gani miradi hiyo inatekelezwa ambapo Wakazi wa Kijiji cha Buyagu walipata fursa ya kuiomba serikali kusimamia vyema mradi wa maji wa Buyagu-Kalangalala-Bitoto ili ukamilike kwa wakati na kuwawezesha kupatana kwa maji safi na salama.
Wakazi hao waliyasema hayo jana baada ya Kamati ya Siasa (CCM) Mkoa Mwanza ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt.Antony Diallo ili kujionea utekelezaji wa mradi huo ambao ulianza tangu Januari 2014 ukitekelezwa na kampuni ya “D4N Co. Ltd” kwa gharama ya shilingi bilioni 1,702,500,170.
Mkandarasi wa mradi huo wa maji ambao chanzo chake ni maji ya Ziwa Victoria alieleza kwamba umechelewa kukamilika kutokana na ucheleweshwaji wa fedha ambapo hadi sasa fedha zilizotolewa na serikali ni shilingi milioni 661,648,480 sawa na asilimia 70 ambapo ukikamilika utawahudumia zaidi ya wakazi 16,000 waishio Vijiji vya Buyagu, Kalangalala na Bitoto.
Pia kamati hiyo ilitembelea uboreshaji wa mradi wa maji katika eneo la Busisi ikiwa ni pamoja na ufungaji wa Pambu mpya ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa Dkt.Antony Diallo amepongeza hatua iliyofikiwa na mkandarasi katika mradi huo huku akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili kutoa huduma kwa wananchi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.