Baadhi ya wazazi na walezi kutokuwa na uelewa juu ya dhana halisi ya Elimu Bure, hali hiyo imesababisha kushuka kwa ufaulu wa mitihani ya sekondari na shule za msingi kwa mwaka 2016 kwa asilimia 6 wilayani Sengerema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sengerema Ndg. Magesa Mafuru Boniphace, Oscar Kapinga kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Sengerema amewaomba wazazi waondokane na mtazamo kuwa elimu bure ndiyo mwanya mkubwa wa wazazi kutowanunulia mahitaji muhimu ya shule watoto wao kwani jambo hilo linapelekea watoto wengi kutohudhuliwa masomo ipasavyo na kudidimia ufaulu kwa wanafunzi.
Kikao hicho chenye lengo la kujadili namna ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Sengerema, kimehudhuliwa na wadau wa elimu, maafisa elimu wa shule zote na wakuu wa shule za msingi na sekondari.
Katika hatua nyingine Kapinga amesema kutokana na hali ya ufaulu kwa mwaka 2016 kushuka kwa asilimia 6 , kikao hicho ana imani kitasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kiwango kikubwa kutokanana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikikwamisha ufaulu kwa wanafunzi kujadiliwa.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.