Walengwa wanaonufaika na mpango wa TASAF kunusuru kaya masikini awamu ya tatu wametakiwa kuunda vikundi vya ujasiliamali ili kujikwamua na umasikini ili hata mpango huo utapomalizika wawe na uwezo wa kujitegemea na kuendeleza maisha yao ya kila siku.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Sengerema Ndg. Charles Kiula alipokuwa katika kijiji cha Mayuya kata ya Tabaruka, alipotembelea kujionea shughuli za uhawilishaji fedha kwa walengwa wanaonufaika na mpango.
Amesema kuwa TASAF imewahimiza walengwa kuunda vikundi vya ujasiliamali ili waweze kujitegemea na vikundi hivyo vitaundwa kila eneo waliopo walengwa na vikundi vinavyotakiwa kuundwa ni pamoja; ufugaji wa kuku, bustani za mbogamboga na ufugaji wa mbuzi lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujitegemea bila kusubili msaada.
Ndg. Kiula amesema kuwa katika maeneo mbalimbali vikundi hivyo vimeanza kuundwa na wataalamu kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wilaya ya Sengerema wataanza zoezi la kutoa elimu ya mafunzo ya ujasiliamali kwa walengwa, kuanzia wiki ijayo na amewataka walengwa hao kujitokeza kwa wingi katika mafunzo hayo ili wapate elimu hiyo.
Frola Medadi ni mlengwa katika mpango wa kunusuru kaya masikini katika Kijiji cha Mayuya Kata ya Tabaruka Wilayani Sengerema ana familia ya watoto saba na mme wake wanapokea shilingi 36,000 lakini wameweza kujikwamua na umaskini kutokana na fedha hizo kwa kujenga nyumba moja ya bati ya vyumba vitatu na kuanzisha ufugaji wa kuku. Pia wametumia nafasi hiyo kutoa pongeza kwa serikali juu ya mpango wake huu wa kunusuru kaya masikini kwani kwaoumekuwa mkombozi mkubwa na jamii nzima kwa ujumla kwani hali ya utegemezi imepungua sana.
Huku Ndg. Edwin Itamba ambaye ni kaimu Afisa Elimu Shule za msingi wilayani Sengerema amewataka walengwa wanaopata fedha kwa ajiri ya kusomesha watoto wazitumie kama zilivyokusudiwa ili watoto hao wapate elimu iliyobora kwa maisha yao ya baadaye.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.