Huduma ya Maji Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza imelejea baada ya ukimya wa mda mrefu, jana majira ya saa tano usiku na jamii ya Sengerema kulipuka kwa furaha tangu kulejea kwa huduma hiyo.
Mmoja wa wananchi mjini humo Bwn. Amos Ramadhani amesema yeye alipokuwa nyumbani kwake majira ya saa nne usiku alipona bomba lake likitoa maji alistaajabu juu ya swala hilo ambalo waliliona kama ndoto.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Bwn. Magesa Mafuru ambaye yuko mjini Dodoma alipokuwa amekwenda kufuatilia swala hilo na kufanikiwa kujerejeshwa kwa huduma hiyo, amesema mazungumuzo yalifanyika na wizara tatu husika ambazo ni Wizara ya TAMISEMI , Nishati na Wizara ya Maji pamoja na viongozi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na viongozi wa Halimasahuri yamefanikisha kurejesha huduma ya maji sengerema.
Kuhusu deni la Shilingi milioni 200 wanalodaiwa mamulaka ya maji safi mjini Sengerema (SEWASA) na TANESCO kama limelipwa alisema kuwa yeye anachofahamu, juu ya urejeshwaji wa huduma ya maji na mambo mengine serikari inafahamu. Amewawaomba wananchi wa sengerema kuendelea kulipa bili ili kutunisha mfuko wa Seuwasa na kazi
Alisema mazungumuzo yalifanywa na wizara tatu husika ambayo ni Tamisemi , Nishati na wizara ya maji pamoja na viongozi wa shirika lamume Tanzania Tanesco pamoja na viongozi wa halimasahuri yamefanikisha kurejesha huduma ya maji sengerema.
Kuhusu deni la sh.miloni 200 wanalodaiwa mamulaka ya maji safi mjini Sengerema (SEWASA) na TANESCO kama limelipwa au raha ! amesema kuwa yeye anachofahamu ni kufuatilia urejeshwaji wa huduma ya maji na mambo mengine Serikari inafahamu, pia amewaomba wananchi wa sengerema kuendelea kulipa bili ili kutunisha mfuko wa SEWASA ili mradi uendelee kujiendesha.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mwl. Emmanuel wakati akizindua zoezi la upandaji miti leo mjini Sengerema amewahakikishia wananchi wa Sengerema kuwa maji yamerejea na hayata katwa tena na mazungumuzo hayo ya kuhusu deni hilo yamekamilika.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.