Ujio wa Kivuko kipya cha MV. Mwanza ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa alipokuwa anagombea kiti cha urais awamu ya tano mapema mwaka 2015. Mv Mwanza ilianza kujengwa mapema mwanzoni mwa mwaka 2015 chini ya mkandalasi wa kitanzani ‘Songoro Marine Transport’ kwa gharama ya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 8.9
Kivuko hiki kinafanya kazi kati ya kigongo na busisi na kinatoa huduma kwa kuunganisha mkoa ya Mwanza, Geita na mikoa jirani. Kivuko hiki kimekuwa msada na mkombozi mkubwa kwa wakazi wa maeneo husika hasa katika utekelezaji wa zana nzima ya “Hapa kazi tu” kwani kimeweza kutatua kero ya usafiri iliyokuwepo kwa mda mrefu iliyokuwa inasababishwa na kuharibika mara kwa vivuko vilivyokuwepo hapo awali.
Jambo ambalo lilidumaza ukuwaji wa uchumi na kasi ya maendeleo miongoni mwa wananchi wa maeneo husika ambao wamekuwa wakitumia usafiri huo wa kivuko kama kiunganishi kikuu kati ya Mwanza, Geita na mikoa jirani, kwani iliwalazimu kutumia masaa kadhaa au mda mwingine siku kadhaa kwa lengo la kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Aidha ujio wa kivuko hiki kipya umekuwa mwarobaini wa kero hiyo kwa wananchi kwani hivi sasa wananchi wanatumia kivuko kipya ambacho kimsingi kinatumia mwendo wa dakika 10 hadi 15 kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine kitu ambacho ni historia tangu kupata uhuru na kinauwezo wakubeba magari 36 na watu 1,000 kwa wakati mmoja.
Hata hivyo serikali bado inaendelea na mikakati mbalimbali ili kumaliza kabaisa tatizo la usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo kama ambavyo Eng. Ramadhan Ally amabye ni msimamizi wa kivuko cha Kigongo - Busisi anaelezea “kwa mwaka huu wa fedha Serikali imejipanga kukipeleka matengenezo kivuko chake cha MV Sengerema na mwakani kivuko kikingine MV Misungwi tutakipeleka matengenezo lengo ni kumaliza adha ya usafiri kwa wakazi wa Mwanza, Geita na mikoa jirani”
lakini jambo linguine niwaombe wakazi wa maeneo ya jirani na watumiaji wa kivuko hiki kuwa walinzi wa mali hizi za serikali dhidi ya watu ambao hawana nia njema na juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
|
|
Hata hivyo Serikali kupitia malengo yake ya mda mrefu ina mpango wa kujenga daraja kati ya Kigongo na Busisi jambo ambalo pindi litapokuwa limekamilika ni dhahili kuwa adha kivuko kati ya Mwanza, Geita na mikoa jirani litakuwa limekwisha kabisa.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.