Zaidi ya vikundi kumi na mbili vya wanawake na vijana katika Halmashauri ya wilaya ya Sengerema, vimepokea kiasi cha shilingi milioni 10 ikiwa ni fedha kutoka katika makusanyo ya ndani, kama ambavyo sera ya serikali inaagiza lengo ikiwa ni kuondoa umaskini kwa makundi ya vijana na wanawake nchini.
Akikabidhi fedha hizo Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Ndg. Emanuel Kipole, amewataka vijana kuachana na makundi mabaya hasa vitendo vya uvutaji bangi, uchezaji pool, bali muda huo wautumia kufanya shughuli za kuwaongezea kipato ikiwa na pamoja na kujishughulisha na kilimo.
Pia amewataka akina mama waliopata fedha za mfuko wa wanawake kuachana na dhana ya kuwa tegemezi (gori kipa) kwa wanaume zao kwani jambo hilo la kuwa tegemezi si kwamba linawaondolea dhana ya usawa bali limekuwa likisababisha migogoro mingi ndani ya familia kwani, amesema “wanawake wengi mmeonekana kuwa mzigo mbele za waume zenu, sasa kupitia fursa hii mliyoipata ni dhahiri kuwa hata amani ndani ya familia itaongezeka iwapo tu kila mmoja atakuwa na shughuli ya kumuigizia kipato na hivyo kila mmoja kuwa tegemezi kwa mwenzake”
Akihitimisha Mhe. Mkuu wa wilaya amevitaka vikundi vyote vilivyopata fedha katika mfuko wa vijana na wananwake kuhakikisha wanafanya marejesho kwa wakati na kuvionya vikundi vyote ambavyo havijarudisha fedha hizo kuhakikisha vinafanya hivyo mara moja tofauti na hivyo atavichukulia hatua za kisheria kwani fedha hizo hazikutolewa kama sadaka bali ili fedha hizo ziweze kuzungushwa na makundi mengine ya vijana na wanawake waweze kunufaika na mfuko.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Magesa Mafuru Boniphace ameahidi kila robo ya mwaka fedha za mfuko wa vijana na wanawake zitakuwa zinatolewa kwa wakati katika vikundi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.