Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza imefanikiwa kutatua tatizo la vitabu kwa darasa la kwanza hadi la tatu kwa kutoa vitabu kwa uwiano unaotakiwa kwa mjibu wa serikali. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongera katika hafra fupi ya uzinduzi wa utoaji vitabu shule za msingi ,uliofanyika katika shule ya msingi Pambalu wilayani hapa.
Mh.Kipole amebainisha kuwa, kupatikana kwa vitabu hivyo watakuwa wamefanikiwa kufikia lengo kwa darasa la kwanza hadi la tata ambapo kila mwanafunzi atakuwa na kitabu chake. Aidha, Mhe. Kipole amesema jumla ya vitabu elfu sitini na tano mia tano thelathini na mbili( 65,532) vya darasa la kwanza hadi la tatu vyenye thamani ya shilingi Millioni miatatu na tisini na tatu mia moja tisini na mbili vimetolewa na serikali.
Nae Afisa elimu shule ya msingi Wilayani Sengerema Bw. Osca Kapinga akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya sengererma ina jumla ya shule 98 za serikali zitanufaika na vitabu hivyo.
Hata hivyo serikali imekusudia kutatua tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za msingi ili kutimiza ahadi yake ya elimu bila malipo na kuongeza ufauru kwa wanafunzi.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.