Halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza imefanikiwa kufufua huduma ya josho la kuogesha mifugo katika kata ya Kagunga lililopo katika kijiji cha Lwenge baada ya kukwama kutoa huduma hiyo kwa muda wa miaka 4 kutokana na miundombinu ya josho hilo kuharibika .
Akitangaza kufufua huduma hiyo kaimu mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya Sengerema Bwn. Malissa Ndugha amesema kuwa wamerejesha huduma hiyo baada ya serikali na wadau wengine wa maendeleo kukarabati miundombinu ya josho hilo na kuwataka viongozi wa serikali ya kijiji cha Lwenge kutoligeuza josho hilo kuwa sehemu ya mtaji wao.
Naye mratibu wa shirika la DALBERG linalojihusisha na masuala ya kilimo na mifugo katika halmashauri za na Sengerema Bwn. Samson Erasto Misambo akitoa taarifa fupi ya gharama za ukarabati wa josho hilo amesema shirika hilo limefadhili zaidi ya milioni moja kwa ajili ya ukarabati na wananchi wa eneo hilo wamechangia nguvu zao kwa kusomba mchanga pamoja na kokoto.
Kwa upande wao viongozi wa serikali ya kijiji cha Lwenge na baadhi ya wafugaji wa eneo hilo wameishukru serikali kwa kurejesha huduma hiyo kwani itawasaidia kuogesha mifugo yao na kuwakinga dhidi ya wadudu wanaoshambulia mifugo yao huku wakiahidi kuimarisha ulinzi katika josho hilo.
Aidha Josho hilo tayari limeanza kutoa huduma ya kuogesha mifugo katika vijiji vya Lwenge , Nyanchenche , Nyanzumla na kagunga .
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.