Mradi mkubwa wa maji Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza unatarajiwa kukamilika machi 31 mwaka huu.(2017)
Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza Injinia Sanga baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema.
Mradi huo umegharimu dola za kimarekani milioni 30.4 ambapo kwa sasa hatua ya iliyobaki ili kukamilisha mradi huo ni kuweka mchanga pekee.
Waziri wa kilimo na umwagiliaji mh,Gerson Lwenge ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Sengerema kwa jitihada walizozifanya kufikisha katika hatua nzuri mradi huo wa maji na kusema kuwa wizara yake inahitaji ifikishe maji vijijini kwa asilimia 85 na asilimia 95 kwa maeneo ya mijini ifikapo mwaka 2020.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bwn,Emmanuel Enock Kipole ameipongeza serikali na Wizara ya maji na umwagiliaji kwa kusaidia kuwezesha mradi huo mkubwa wa maji kwani suala la maji katika wilaya ya Sengerema litabaki kuwa historia mradi utakapokamilika.
Ziara ya waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh,Gerson Lwenge imeambatana na kamati ya Bunge ya kilimo na umwagiliaji pamoja na maafisa wa sekta mbalimbali serikalini.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.