Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Binuru Shekidele amewasisitiza watoa huduma kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuhakikisha wanatoa huduma bora za afya sambamba na kuzingatia usafi katika maeneo ya vituo hivyo.
Shekidele ameyasema hayo leo (Julai 15, 2024) wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utoaji wa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mwabaluhi pamoja na vituo vya afya vya Buzilasoga na Nyamazugo ambacho kipo katika hatua za ukamilishaji ili kianze kutoa huduma.
Amesema watumishi waliopo katika maeneo hayo wanapaswa kulinda rasilimali zote zilizopo katika vituo hivyo sambamba na itoaji wa huduma bora kwa wananchi .
Akikagua zoezi la usafi na ufungaji wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ya Mwabaluhi, Shekidele amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri kuhakikisha zoezi la uwekaji wa njia za watembea kwa miguu ndani ya hospitali hiyo, ufungaji wa vitanda pamoja na ukamilishaji wa vifaa mhimu linapewa kipaumbele ili hospitali hiyo iweze kuanza kutoa huduma haraka iwezekanavyo.
Mapema akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Nyamazugo Shekidele amemwagiza fundi anayejenga kituo hicho kukamilisha kazi hiyo katika ubora huku akimtaka kuhakikisha dosari zote zilizipo katika baadhi ya majengo hayo zinarekebishwa ili kituo hicho kianze kutoa huduma haraka.
Kwa upande wa kituo cha afya cha Buzilasoga, Shekidele amemwagiza Mganga mkuu wa Halmashauri kuhakisha huduma za maji zinapatikana haraka ili kusaidia kituo hicho ambacho kimeanza kutoa huduma kwa wanachi wa kata hiyo ambapo amesema kipaumbele kikubwa kwa sasa katika kituo hicho ni upatikanaji wa maji ya uhakika ili kuondoa usumbufu kwa watumishi na wagonjwa wa kituo hicho.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.