• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DC SENGEREMA ATOA ONYO KALI WATAKAOPUUZA KIDATO CHA KWANZA 2023

Posted on: December 28th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga ametoa onyo kali kwa wazazi au walezi watakao shindwa kuwapeleka watoto wao kujiunga na kidato cha kwanza mwezi Januari 2023 kwani Serikali imejenga madarasa ya kutosha katika shule za Sekondari.


Mkuu wa Wilaya ametoa onyo hilo leo Disemba 28, 2022 wakati wa hafla ya ya makabidhiano ya ujenzi wa vyumba 152 vya madarasa ya Sekondari iliyofanyika Sekondari ya Nyampulukano katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.


Mkuu wa Wilaya amesema, hivi sasa Serikali imejenga na kuweka miundombinu ya kutosha katika shule za sekondari hivyo hakuna sababu ya wazazi kushindwa kuwapeleka watoto kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwezi Januari 2023.


"Mtoto ambaye amepangiwa kwenda kidato cha kwanza mwaka huu ni lazima aende, mtoto asipoenda shule wakati madarasa tena yenye madawati yameandaliwa huo ni uhujumu uchumi na mwaka huu lazima tutoe mfano kwa wazazi wote watakao kaidi kupeleka watoto kidato cha kwanza na ninamanisha katika hili" amesisitiza Mkuu wa Wilaya.


Mhe. Mkuu wa Wilaya mbali na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo kwa wakati, amewaomba wadau mbalimbali  kujitokeza kuwasaidia watoto wenye uhitaji waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kwa kuwasaidia baadhi ya mahitaji ikiwemo madaftari na mahitaji mengine ya mhimu ili wote waweze kuanza masomo kwa wakati.


mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Mhe. Yanga Makaga amepongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwani kupitia fedha hizo zimekamilisha ujenzi wa vyumba hivyo pasipo kuchangisha fedha kwa wananchi.


Awali akitoa taarifa juu ya ujenzi wa vyumba hivyo, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ndugu Mwita Waryuba amesema ujenzi wa vyumba hivyo ulianza mwezi Oktoba 2022, ambapo hadi sasa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ni vyumba vya madarasa 8 tu ambavyo havijakamilika kati ya vyumba 152.


Kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo 152 yaliyojengwa kwa shilingi 3,040,000,000 kunaifanya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari.

Matangazo ya Kawaida

  • TAARIFA YA FEDHA YA HESABU ZA MWISHO HALMASHAURI YA WILAYA SENGEREMA KWA MWAKA ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI 2024 August 06, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI MBALIMBALI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA July 29, 2025
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA NYONGEZA KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA NYANZAGA MINING COMPANY LIMITED KWA AJILI YA UCHIMBAJI MKUBWA WA MADINI YA DHAHABU

    August 20, 2025
  • MAADHIMISHO YA KILELE CHA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA

    August 20, 2025
  • MAFUNZO KWA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA

    August 04, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKIZI YA MAUAJI YA WATU WENYE UALBINO

    July 29, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.