Pikipiki 26 zenye thamani ya shilingi milion 78 zilizotolewa na serikali kwa Halmashauri ya Sengerema zimekabidhiwa kwa Waratibu Elimu Kata ili kusimamia utekelezaji wa sera ya Elimu katika Halmashauri hiyo. Alipokuwa akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh. Emmanuel Kipole amewataka Waratibu Elimu hao kutumia pikipiki hizo katika kukagua utekelezaji wa Sera ya Elimu na uboreshaji wa kiwango cha ufaulu wilayani humo.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Magesa Mafuru Boniface amewaasa waratibu kwa kusema, “ kupatikana kwa pikipiki hizo ni hatua kubwa katika utekelezaji wa Sera ya Elimu hivyo mnapaswa kuhakikisha kila mwanafunzi anajua kusoma na kuandika”.
Kwa upande wa waratibu walipokea pikipiki hizo wameipongeza serikali kwa kuwapatia vitendea kazi hivyo na kwamba maelekezo na maagizo yote ya serikali yatazingatiwa kwakuwa wanaouwezo sasa wa kufika kila eneo ambalo mwanzo walipata shida kulifikia.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.