• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

DARAJA LA MAGUFULI KUANZA KUTUMIKA DISEMBA 30, 2024

Posted on: July 3rd, 2024

Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo – Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3.0 na barabara unganishi Kilomita 1.66 linatarajiwa kuanza kutumika Tarehe 30 Disemba 2024 likiunganisha Barabara Kuu ya          Usagara – Sengerema – Geita zenye urefu wa Kilomita 90.



Daraja hilo linajengwa Urefu wa kilometa 3.0 Upana meta 28.45; unaojumuisha njia mbili (2) za Magari (Carriageways) zenye upana wa meta 7.0 kila upande, njia ya maegesho ya dharura meta 2.5 kila upande, njia za watembea  kwa miguu (Walkways) meta 2.5 kila upande, eneo la kati linalotenganisha  uelekeo tofauti wa barabara (Median) meta 2.45, kingo za magari (GuardRails Kerbs) meta 0.5 kila upande, na kingo za watembea kwa miguu (HandRails Kerbs) meta 0.5 kila upande.



Akizungumza mara baada ya kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa daraja hilo Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS Mkoa wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose amesema kuwa daraja hilo linajengwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation ikishirikiana na China Railway 15 Bureau Group Corporation (CCECC - CR15G JV) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 592.6 bila 18% VAT.



Amesema kuwa kwa ujumla Mradi huo umeshatoa jumla ya ajira 29,211 tangu kuanza kwake tarehe 25 Februari 2020 ambapo asilimia 93.33 sawa na ajira 27,262 ni Wazawa na ajira 1949 sawa na asilimia 6.67 ni Wageni.



Amebainisha kuwa Utekelezaji wa Mradi huo umefikia asilimia 88.61 dhidi ya 91.70% ya Mpango kazi Na. 5 ulioidhinishwa huku Vifaa na mitambo ya ujenzi vilivyofika eneo la kazi hadi sasa vimefikia asilimia 99.



Mhandisi Ambrose amezitaja faida zitakazopatikana baada ya kukamilika kwa daraja hilo kuwa ni pamoja na kupunguza muda wa kusafiri na uwepo wa uhakika wa usafiri masaa 24, kuondoa msongamano wa magari uliokuwa unatokea kwenye feri, Litakuwa kiungo muhimu kwa Mkoa wa Mwanza na Mikoa inayouzunguka pamoja na Nchi  Jirani na pia Daraja hilo litakuwa kivutio muhimu kwa Mkoa wa Mwanza na ni nembo kwa nchi ya Tanzania.



Mhandisi Ambrose ameeleza kuwa Usanifu wa daraja hilo umetumia teknolojia ya madaraja marefu (Long Span Bridges), inayoitwa “Extra Dosed Bridge” ambapo kutakuwa na Nguzo Kuu (Pylons) tatu (3) zenye kimo cha mita 40 na umbali mita 160 kutoka nguzo moja hadi nyingine.



Amesema Daraja litakuwa na nguzo nyingine 64, ambapo 2 kati ya hizo zitakuwa umbali wa mita 100  kutoka nguzo moja hadi nguzo kuu wakati zilizobaki zitakuwa umbali wa mita 40 kutoka nguzo moja hadi nyingine na Jumla ya nguzo katika daraja lote zitakuwa ni 67.



Kila Nguzo ya Daraja ina nguzo za msingi (pile foundations) zilizochimbiwa ardhini kwa urefu wa kati ya mita 11.5 na mita 66, vilevile kutakuwa na Barabara unganishi yenye njia mbili zenye upana wa mita 7 kila upande kwa  ajili ya magari na mabega ya mita 2.5 kila upande wa barabara zenye jumla ya urefu   wa kilometa 1.66 (Upande wa Kigongo kilometa 1.16 na upande wa Busisi mita 500).

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.