Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema leo (28.05.2024) imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri.
Wakikagua hospitali ya Halmashauri iliyopo Mwabaluhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri amemwagiza Mganga Mkuu pamoja na uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha usafi wa mazingira katika eneo lote la hospitali unapewa kipaumbele pamoja na maboresho ya njia zinazounganisha majengo yote katika hospitali hiyo zinatengenezwa haraka ili hospitali hiyo ianze kutoa huduma katika maeneo yote.
Miradi mingine iliyotembelewa na Timu ya Menejimenti ni pamoja na Ujenzi wa Bweni la wanafunzi la shule ya Sekondari Mwabaluhi ambalo linajengwa kwa nguvu za wananchi, Ujenzi wa darasa shule ya msingi Mweli pamoja na jengo la Utawala lililopo Bomani.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.