Akizindua kampeni hiyo Mhe. Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndg. Hamis Mwagao Tabasamu amewataka vijana, wananchi pamoja na wakazi wote wa Sengerema kuondokana na dhana potofu inayotolewa na watu kwenye mitandao dhidi ya Chanjo ya UVIKO 19
Amesisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inalinda afya ya wananchi wake hivyo wasiwe na hofu kwani chanjo hiyo ni salama na wataalamu wetu wa afya wamejiridhisha kuwa ni salama.
Mganga mkuu wa wilaya Dr. Saumu Kumbisaga amewataka makundi yote lengwa kujitokeza kupata chanjo hiyo na vituo vitakavyotumika kutoa chanjo hiyo ni Kituo cha Afya Sengerema, katika Hospital Teule ya DDH, kituo cha Afya Kahunga kilichopo kata ya Ngoma A, Busisi Dispensary pamoja na Kituo cha Afya Katunguru
Nae Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Nganga amewaasa wananchi kuchangamkia fursa hii ambayo Serikali imeambua kuingia gharama ili iweze kulinda usalama wa wananchi wake.
Hata hivyo amesisitiza kuwa yeye kama msimamizi mkuu wa serikali katika wilaya ya Sengerema hata sita kumchukulia hatua mtu yeyote atakaye onekana anapotosha umma kwa makusubi, huku akiwakumbusha wananchi kwa kusema, “ndugu zangu chanjo hii ni hiari yako hivyo asitokee mtu amekuja kukulazimisha”
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.