hiKamati ya mradi wa kuimarisha na kuboresha elimu ya Awali na Msingi (BOOST) wilayani Sengerema imewaasa mafundi na wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika miradi hiyo kuhakikisha wanasimamia vyema suala la usalama wao na mazingira wawapo kwenye eneo la mradi.
Hayo yamebainishwa leo jumamosi Mei 13 wakati kamati hiyo ilipotembelea kwenye maeneo ya miradi ya BOOST kwa lengo la kutoa elimu ya usalama wa mafundi na wasimamizi wawapo kazini pamoja na kubaini mipaka ya maeneo hususan mahali ambapo zinajengwa shule mpya za msingi za Kilabela na Bugumbikiso kupitia mradi wa BOOST.
Afisa elimu Msingi wa Halmashauri ndugu Donati Bunonos amesema miongoni mwa vigezo mhimu vya mradi wa BOOST ni usalama wa mafundi wawapo kazini hivyo kamati hiyo inalojukumu ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wote wanahosika na mradi huo.
"Najua tunafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi hivyo kamati hii imefika hapa kuwaeleza mambo mhimu ya kuzingatia tunapokuwa kwenye eneo la mradi" amesema Afisa elimu msingi.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ndugu Wilbard Muyumbu amewataka mafundi hao kuhakikisha wanazingatia utunzaji wa mazingira ikiwemo matumizi ya vyoo wawapo katika eneo la mradi pamoja na mavazi maalumu yatumikayo wakati wa ujenzi kama vile uvaaji wa kofia ngumu, gloves na Gambuti.
Mwakilishi wa idara ya Maendeleo ya Jamii ndugu George Adolph amewaasa mafundi hao kuhakikisha wanazingatia usalama, afya na mazingira ya mradi pamoja na wadau wote wanaozunguka eneo la mradi hivyo amewataka mafundi hao kufanya kazi huku wakiweka mbele usalama wa afya zao na mazingira yanayowazunguka.
Mradi wa BOOST katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema unatekelezwa katika jumla ya shule 10 kwa gharama ya shilingi 1,606,400,000 ambapo kuna miundombinu mbalimbali imeanza kujengwa katika shule hizo.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.