Akiwasilisha Mpango huo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Mkuu wa Idara ya Mipango Bw. Samson Ndaro kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. Magesa Mafuru Boniface alisema, Halmashauri inakadilia kukusanya na kupokea mapato yenye jumla ya Shil. 55,381,201,248.00 ikiwa na ongezeko la 17.2% zaidi ya ile ya mwaka 2018/2019 ambayo ilikuwa ni Shil. 45,346,793,053.49. Bajeti imezingatia mahitaji yote mhimu kwa ajili ya ustahimili wa Halmashauri hasa matakwa ya kisheria yanayopashwa kutekelezwa kama vile ailimia 2% kwa ajili ya watu wenye ulemavu, 4% wanawake na 4% vijana ambapo zaidi ya Mil. 100 zimetengwa kwa ajili ya makundi hayo. Pia ukamilishaji na uanzishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kutokana na 40% ya makusanyo ya ndani.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw, Yanga Makaga, alipokuwa akitoa hutuba yake wakati akihairisha Baraza ameahidi kusimamia kwa kikamilifu utekelezaji wa Bajeti hiyo kwani bajeti hiyo inakwenda kukamilisha au kumaliza kero za wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri yetu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.