KUPATA KIBARI CHA KUMILIKI SIRAHA
1. Mwombaji unatakiwa kuandika barua ya maombi kupitia ofisi ya kijiji au mtaa juu ya kusudio lake hilo la kuomba kumiliki siraha.
2. Ofisi ya kijiji au mtaa itaandaa mkutano mkuu wa kijiji au mtaa ambapo mkutano huo mwenyekiti wake atakuwa mwenyekiti wa kijiji au mtaa na katibu wa mkutano huo atakuwa ni mtendaji wa kijiji au mtaa. Agenda ya mkutano huo itakuwa ni kumjadili mhusika au mwombaji anayetaka kumiliki siraha kama ni mtu amabaye hana kashifa mbaya kama wizi au ujambazi katika mtaa au kijiji husika. Mkutano mkuu ukiridhia hana matatizo basi ataandikiwa barua ya kumtambulisha mbele ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
3. Mkuu wa Wilaya baada ya kupokea barua hiyo ya utambulisho toka ofisi ya kijiji au mtaa juu ya jambo tajwa toka kwa mwombaji atakaa na kamati yake ya ulinzi na usalama kisha watajiridhisha na baadae watatuma maombi hayo kwenda mkoani.
4. Ofisi ya mkuu wa mkoa nayo itapitia na kamati ya ulinzi na usalama mkoa na baada ya kujiridhisha basi itatoa kibari cha kumiliki siraha kwa mwombaji.
NB:
IKITOKEA MWOMBAJI AMEPATA KIBARI BASI SIRAHA UNAYOIOMBA UTATAKIWA KUINUNUA NA BAADA YA HAPO UTATAKIWA KUWA UNAILIPIA LESSENI YA KUMILIKI SIRAHA HIYO KILA MWAKA
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.