Tuesday 3rd, December 2024
@NYAMAZUGO
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuri anataraji kuwasiri wilayani Sengerema Julay 4 majira ya saa mbili asubuhi kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo kilichopo katika chanzo cha mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana amesema kuwa Rais atakapokuwa wilayani Sengerema atafanya kazi moja ya kuzindua mradi mkubwa maji ambao utawahudumia wakazi wa sengerema zaidi ya watu 130,000
Amesema akiwa njiani kuelekea katika tukio la kuzindua mradi huo atasalimiana na wananchi barabarani kadri itakavyowaezekana na baada ya kuzindua mradi huo atawahutubia wananchi wa sengerema na viunga vyake hivyo amewataka wananchi kujitokeza na kumraki mhesimiwa Rais atakapowasili.
Kipole amesema wilaya ya Sengerema inajumla ya wakazi laki 74,186 kutokana na sense ya watu na makazi ya mwaka 2002 hivyo mradi huu kwa sasa utahudumia kata zipatazo tisa zinazounda maamuraka ya mji wa sengerema ambazo ,Nyamazugo Sima, Nyatukala, Ibisabageni, Mwabaruhi, Nyampulukano, Misheni, Tabaruka, Nyampande Ibondo na Nyamizeze ambapo huduma ya maji itawafikia wakazi wa sengerema wapatao zaidi ya 20, 000 na kuwaondolea adha ya maji wananchi hao.
Injiana wa maji wilaya ya Sengerema Nikas Ligombi amesema mradi huu wa Bilioni 23 ulianza mwaka 2014 ambapo ulifadhiwa na Benki ya Afrika na umekamilika kwa asilima 100 ambapo mtambo huo utakuwa na uwezo wa kusukuma lita za ujazo 1,500,000 kwa siku na hivyo ni imani yangu kuwa mradi huu utakapo zinduliwa na Mheshimiwa Rais tatizo la maji katika mji wa Sengerema litakuwa limepatiwa ufumbuzi na kuwa historia.
Mkuregenzi wa Halimashauri ya Sengerema Magesa Mafuru amesema kuwa nifahari kubwa kukamlika kwa maradi huu ambao utamaliza tatizo ya maji lililokuwa likiukumba mji wetu wa sengerema, na hivyo kuwataka wananchi kuutunza na kuuthamini ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.