Halmashauri ya Sengerema inakadiriwa kuwa na idadi ya Mifugo kama ifuatavyo; Ngo’mbe 152,600, Mbuzi 135,404, Kondoo 6,860, Kuku 366,278, Nguruwe 2,591, Punda 42, Mbwa 9,078 Paka 8,291, Bata wa kawaida 68,752 na Bata Mzinga 189. Idadi ya majosho 22 yanayotumika ni 10 tu, Machinjio ndogo (Slaunghter slab) 8, vibanio 3, minada ya Ng’ombe 2 na Minada ya Mbuzi 3.
Halmashauri inakadiriwa kuwa na mitumbwi ya kasia 797, mitumbwi inayotumia mashine 352 na wavuvi 3,799. Shughuli za uvuvi zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wavuvi juu ya umuhimu wa kutunza rasilimali za uvuvi na kuwa endelevu kwa kizazi cha leo na kijacho kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla. Pia shughuli za ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba unaendelea katika Halmashauri ya Sengerema ambapo jumla ya vikundi 5 na Watu binafsi 2 wamenufaika na mikopo ya Benki ya Kilimo.