Halmashauri ina hifadhi za misitu ya miti asili 3 zenye ukubwa wa Hekta 105 inayomilikiwa na serikali za vijiji vya Ilekanilo, Kasomeko na kitongoji cha Bomani. Pia msitu wa kupandwa wenye ukubwa wa Hekta 882 unaomilikiwa na Halmashauri katika kijiji cha Nyamahona. Zoezi la uoteshaji miche 67,786 katika kitalu cha kikundi cha Bwawani na TFS Sengerema miche 982,214 ambayo kikundi huuza na TFS hugawa bure kwa wananchi na Taasisi za Umma. Uhamasishaji wa upandaji wa miti umefanyika hadi mwezi Mei 2023 ambapo miche 1,050,000 imepandwa na watu binafsi na taasisi ambayo ni sawa na asilimia 70 ya lengo la miti 1,500,000 la kila mwaka.
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.