Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Katika mwaka wa fedha 2022/2023 imepokea Shilingi 1,947,404,930.44 sawa na asilimia 80 kwa mchanganuo ufuatao; Fedha za matengenezo Sh 526,093,043.04, Fedha za Dharura Sh 200,015,000.00 Fedha za Maendeleo ya Jimbo Sh 161,263,959.00, na Fedha za Tozo Sh 1,060,132,928.40. Kazi tekelezwa kupitia fedha hizo ni jumla ya km 203.447, km 0.97 ni za kiwango cha Lami, Km 68.8 za kiwango cha Changarawe, Km 135.4 za kiwango cha udongo, Box Kalavati 11, Kalavati 49 na ujenzi wa mitaro ya mawe mita za ujazo 3659. Jumla ya Miradi 9 inatekelezwa kupitia fedha hizo, ambapo hadi sasa kiasi kilicholipwa kwa miradi yote ni Tsh 1,234,679,610.00
Sengerema District Council
Anuani ya Posta: Box 175
Simu ya Mezani: 028 2590162
Simu: 0688223308
Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz
Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.