• Mawasiliano |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Sengerema District Council
Sengerema District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango na Uratibu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Usafishaji na Mazingira
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Tehama na Takwimu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Manunuzi
      • Mawasiliano Serikalini
      • Fedha na Uhasibu
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasiri na Uhifadhi wa Mazingira
      • Taka ngumu na Usafishaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Biashara
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Majukumu ya Diwani katika Hamashauri
      • Wakuchaguliwa
      • Viti Maalumu
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Ukimwi
      • Elimu, Afya na Maji
      • Maadili
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingizira
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
    • Ratiba ya Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Majukumu ya Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Jarida Tando
    • Nyaraka
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMETEKELEZA MIRADI MINGI SEKTA YA AFYA-DKT. BITEKO

Posted on: November 1st, 2024


Azindua Jengo la Kisasa la Upasuaji Sengerema DDH na Mradi wa Umeme wa Jua

Ahimiza wananchi kutunza miundombinu ya hospitali

Ataja mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sekta ya afya

 Alipongeza Kanisa Katoliki, awashukuru wafadhili wa miradi

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mingi katika sekta ya afya inayolenga  kuongeza ufanisi katika huduma za afya na kuboresha maisha ya Watanzania.


Sambamba na kulipongeza Kanisa Katoliki kwa juhudi zake za kutoa huduma za afya katika maeneo mbalimbali wakati ambao Serikali pia imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya.


Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 1, 2024 Sengerema mkoani Mwanza wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa jengo la jipya la kisasa la upasuaji  na mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya Sengerema DDH iliyopo chini ya Kanisa Katoliki, Jimbo Katoliki la Geita.


Akitaja baadhi ya mafanikio ya Serikali katika sekta hiyo Dkt. Biteko amesema  “ Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia  imefanya kazi nyingi ikiwemo kujenga hospitali mpya 129, kukarabati hospitali kongwe 50, kujenga hospitali za wilaya 677 na zahanati 425. Nawaomba watu Sengerema na sisi wote kwa kujua wafadhili wametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hili na mradi wa umeme wa jua wamejinyima kwa ajili yetu hivyo tutunze miundombinu hii,”


Amesisitiza “Tutatibiwa sisi kutoka Kigoma na Kagera na wakati wa Covid 19 hapa palikuwa na msaada mkubwa haitakuwa sawa wakati mwingine wakija wakakuta tumepabadilisha na kuwa tofauti na lengo lao, tutunze vifaa hivi na majengo haya na tuwape moyo ili waweze kutusaidia katika maeneo mengine yenye uhitaji,”


Ameendelea kwa kuwashukuru wafadhili wa miradi hiyo na kuifanya hospitali hiyo kuwa bora na ya kisasa.“ Tunasheherekea  mafanikio haya kwa sababu umisionari umelenga kuhudumia watu kiroho na kimwili, niwapongeze sana Kanisa Katoliki kwa kuunga mkono juhudi ambazo Serikali ingefanya, pamoja na kuhubiri watu kutenda mema na kuponya magonjwa yao na kuwaondoa kwenye umasikini hilo ni jambo muhimu,”


Aidha, Dkt. Biteko amebainisha kuwa Serikali inathamini mchango wa kanisa katika maendeleo ya watu.


Akizungumzia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2050, amesema inajengwa kwa msingi wa amani na usalama huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na kuwaweka pamoja Watanzania ili waendelee kujenga nchi yao.


Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amewaasa Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani na kufuata taratibu na sheria na kuwa uchaguzi huo usiwe sababu ya kuwagawa.


Naye, Mbunge wa Sengerema, Mhe. Hamis Mwagawa amemshukuru mtawa Dkt. Marie Jose na kumpongeza kwa kutoa huduma kwa wananchi na kusema kuwa hata wakati wa janga la Covid 19 pamoja na kuwashukuru  wafadhili wote waliojitolewa kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la upasuaji.


Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema ujenzi wa hospitali hiyo ulianza kutoka na ujio wa watawa sita na familia moja waliohitaji kujenga hospitali ambayo ingetoa huduma ya afya kwa wahitaji na baadaye hospitali hiyo ikawa teule hadi mwaka huu ambapo Serikali imejenga hospitali yake ya wilaya.


“ Tuna juhudi katika kuendesha huduma kwa gharama nafuu na tuna mfuko wa kusaidia wahitaji ambapo tunapata misaada kutoka Shirika la Marafiki wa Sengerema na Simba Health ambao walikuja na wazo la kuwa na chumba cha upasuaji chenye vifaa vya kisasa na sasa tumepata jengo hili ambalo litasaidia kutoa huduma za kisasa za upasuaji,” amesema  Askofu Kassala.


Ameendelea kusema baada ya kuwa na jengo hilo lilikuja wazo kutoka Shirika la Marafiki wa Sengerema ambao ni madaktari wanafunzi kutoka Uholanzi la kupendekeza mradi wa umeme mkubwa wa jua ili pia usaidie kutumika katika mifumo ya CT scan na MRI.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sengerema Sr. Dkt. Marie Jose amesema kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kulaza wagonjwa 22,000 na inatoa huduma za kibingwa kwa akina mama na watoto pamoja na kuwa sehemu ya kufanya mafunzo kwa vitendo  kwa madaktari wanafunzi kutoka Hospitali ya Kanda ya Bugando.


“ Tumeanza kuboresha huduma zetu na idara ya mionzi ina mitambo mipya, tuna huduma ya watoto wanahohitaji huduma maalum  na tuna umeme wa jua ambao ni wa uhakika. Leo ni siku ya furaha tuna jengo hili ambalo limegharimu shilingi bilioni 2.7 na mradi wa umeme wa jua umegharimu shilingi  bilioni 1.7,” amesema Dkt. Jose.


Moja ya mfadhili wa jengo la upasuaji, Bibi. Doris Mars amesema kuwa walipopata wazo la ufadhili wa mradi huo yeye na familia yake waliamua kusaidia kwa kuwa mradi huo unalenga kuboresha maisha ya watu.


“ Mungu ametupa uwezo wa kusaidia wengine na Biblia Takatifu inatuambia kila binadamu ameumbwa kwa sura na mfano wake hivyo tunaamini tutasaidia kuokoa maisha na kuwapa faraja watu wa Sengerema pia tunawashukuru wote walioto mchango wao katika miradi hii,” amesema Bibi. Mars.


Mwakilishi wa Sopowerful, Dkt. Koen Gelpke amesema kuwa uwepo wa jengo la kisasa ulihitaji pia umeme wa uhakikia ili kutoa huduma kwa wananchi na ndio sababu waliamua kujenga mradi wa umeme wa jua.


Awali Dkt. Biteko ameshiriki katika adhimisho la Misa Takatifu kwa ajili ya ufunguzi wa jengo jipya la kisasa la upasuaji


Akihubiri katika  misa hiyo , Mhashamu Askofu  Mkuu wa Jimbo la Songea, Damiani Denis Dalu amesema kuwa  siku ya leo ni sikukuu ya watakatifu wote na ni sherehe kubwa katika liturijia na kuwa wanawakumbuka  watakatifu wote.


Amefafanua kuwa watakatifu hao ndio waliofaulu na  kuwekwa wafu ili kuwa kuelelezo cha watu  wote kuwa maisha ya kumfuata yesu kristo yana tija mbinguni.


Askofu Dalu ameendelea kusema kuwa Kanisa Katoliki ni la kimisionari ambapo walitumwa mitume 12 dunia kote kwa ajili ya kuhubiri  injili.


“ Wamisionari wa Afrika ndio waliohubiri injili eneo hili katika uinjilishaji wao walihakikisha kila wanapifika wanatoa huduma za afya, elimu na za kijamii kwa ujumla. Na hii ni Parokia ya Bikira Maria Afya ya Wagonjwa eneo hili wamisionari walifungua kituo cha wagonjwa na waliwajengea pia eneo kwa ajili ya kusali.” Amesema  Askofu Dalu.


Amesisitiza “Tunamshukuru Mwasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuenzi na kutambua huduma hizi kwa watu na Serikali kwa kuendeleza hili. Leo tunamshukuru Mungu na tuzidi kuombeana ili hiki tunachoenda nacho kikae sawa, tunashukuru kwa juhudi ambazo Serikali imezifanyq katika hospitali hii mwaka  2013 hadi 2015,”


Pia, Askofu Mkuu Dalu amewashukuru wafadhili kutoka nchini uholanzi kwa mchango wao katika hospitali ya Sengerema DDH “ Tunakoeleka ni kuzuri na tunawashukuru sana  wafadhili wetu kwa  uinjilishaji huu, tunamshukuru pia Askofu kwa urafiki kati ya dayosisi hizi na kutusaidia katika Sengerema Hospitali na kituo cha mafunzo.”


MWISHO

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO AJIRA-UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA September 16, 2024
  • TANAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 26, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI SENGEREMA August 07, 2024
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO ZOEZI UANDIKISHAJI NA BVR August 08, 2024
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • SENGEREMA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MIKOPO YA MILIONI 362

    March 05, 2025
  • UMOJA WA WANAWAKE SENGEREMA WATOA MISAADA

    March 04, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • CHUO KIKUU CHA ARDHI 'KAMPASI' YA SENGEREMA KUANZA KUJENGWA FEBRUARI 2025

    February 03, 2025
  • Ona vyote

Video

DKT. SAMIA AKIWASALIMIA WANANCHI WA SENGEREMA
Video nyingine

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani Yetu
  • Jarida Tando la Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • OR-Tamisemi
  • OR-Ikulu
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani Yetu

Mawasiliano

    Sengerema District Council

    Anuani ya Posta: Box 175

    Simu ya Mezani: 028 2590162

    Simu: 0688223308

    Barua pepe: ded@sengeremadc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faraga
    • Kanusho
    • Ramani Yetu

Copyright ©2021 SENGEREMA DISTRICT COUNCIL . All rights reserved.