Halmashauri ilipanga kukusanya Shs 2,750,000,000/= (2,043,228,000 mapato ya wazi na Tsh 706,772,000 mapato lindwa) kwa mwaka wa fedha 2022/23 fedha za mapato ya ndani. Hadi tarehe 30/06/2023 imefanikiwa kukusanya jumla ya Shs 1,831,168,249.56 sawa na 89% mapato ya wazina Tsh 370,205,260.18 sawa na 52% mapato lindwa hivyo kuwa na jumla ya makusanyo Tsh 2,201,373,509.71 sawa na 80%. Makusanyo haya yameongezeka kutokana na matumizi mazuri ya mifumo inayotumika kukusanyia mapato hasa POS Mashine.